Friday, October 14, 2022

UKUMBUSHO WA IJUMAA


 UKUMBUSHO WA IJUMAA

📚IBADA ZENYE FADHILA ZAIDI SIKU YA IJUMA, BIDAAH ZA SIKU YA IJUMAA NA HATARI YA KUACHA KUSWALI IJUMAA


📚IBADA ZENYE FADHILA ZAIDI SIKU YA IJUMAA


0️⃣0️⃣Kusoma Surah: As-sajidah(Alif laam miim) Rakah ya kwanza na Surah:Al-Insaan(Dahr) Katika rakah ya pili ndani ya swalah ya alfajiri

0️⃣1️⃣KUOGA(𝘄𝗮𝗻𝗮𝘂𝗺𝗲 𝗻𝗮 𝘄𝗮𝗻𝗮𝘄𝗮𝗸𝗲) NA KUJITIA MANUKATO(𝗪𝗮𝗻𝗮𝘂𝗺𝗲 𝗽𝗲𝗸𝗲𝗲 𝘆𝗮𝗼)
0️⃣2️⃣.KWENDA MSIKITINI MAPEMA
📚Amesema Mtume swalallaahu 'alayhi wasallaam:
📚عن أَبِي هُرَيْرَةَ رضي الله عنه قال، أَنَّ رَسُولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم قَالَ: مَنِ اغْتَسَلَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ غُسْلَ الْجَنَابَةِ ثُمَّ رَاحَ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَدَنَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّانِيَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ بَقَرَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الثَّالِثَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ كَبْشًا أَقْرَنَ، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الرَّابِعَةِ فَكَأَنَّمَا قَرَّبَ دَجَاجَةً، وَمَنْ رَاحَ فِي السَّاعَةِ الْخَامِسَةِ فَكَأَنَّما قَرَّبَ بَيْضَةً، فَإِذَا خَرَجَ الإِمَامُ حَضَرَتِ الْمَلاَئِكَةُ يَسْتَمِعُونَ الذِّكْرَ.
📚Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) amesema kwamba Mtume (Swalallaahu 'alayhi wa sallam)amesema: “Atakayeoga siku ya Ijumaa kisha akaenda Msikitini(saa ya kwanza), itakuwa kama mfano ametoa (sadaka ya) ngamia. Akienda saa ya pili yake, itakuwa kama katoa (sadaka ya) nġ’ombe. Akienda saa ya tatu yake, itakuwa kama ametoa (sadaka ya) kondoo mwenye pembe. Akienda saa ya nne yake, itakuwa kama ametoa (sadaka ya) kuku. Akienda saa ya tano yake itakuwa kama ametoa (sadaka ya) yai. Imaam akifika(akipanda mimbari), Malaika watatoka kuja kusikiliza dhikr(khutbab).(Bukhaariy)

🪀Jiunge na Group la WhatsApp la DARUL ILM kisha Rudi nyuma uendelee kusoma
👇👇👇


🤲0️⃣3️⃣Kumswalia Mtume swalallaahu 'alayhi wasallaam siku ya ijumaa kuna fadhila zaidi kuliko siku nyingine
📚 Amesema Allaah Subhaanahu wata'ala:
📚إِنَّ ٱللَّهَ وَمَلَٰٓئِكَتَهُۥ يُصَلُّونَ عَلَى ٱلنَّبِيِّۚ يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُواْ صَلُّواْ عَلَيۡهِ وَسَلِّمُواْ تَسۡلِيمًا
📚Hakika Allaah na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu.(Surah Al-Ahzab, Ayah:56)
📚Katika Ayaah hii, Allaah ametuamrisha kumswalia Mtume swalallaahu 'alayhi wasallaam, na akatanguliza kwanza kuonyesha kwamba yeye mwenyewe Allaah na Malaika wake wanamswalia Nabii. Na hili ni dalili ya kuonyesha ukubwa na utukufu wa ibada hii ya kumswalia mtume swalallaahu 'alayhi wasallaam.
📚Kisha Mtume swalallaahu 'alayhi wasallaam Anasema:
📚عَنْ أَوْسِ بْنِ أَوْسٍ (رضي الله عنه) قَالَ: قَالَ رَسُولُ اللهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ:إِنَّ مِنْ أَفْضَلِ أَيَّامِكُمْ يَوْمَ الْجُمُعَةِ، فَأَكْثِرُوا عَلَيَّ مِنْ الصَّلاةِ فِيهِ، فَإِنَّ صَلاَتَكُمْ مَعْرُوضَةٌ عَلَيَّ.قَالوا: يَا رَسُولَ اللَّهِ وَكَيْفَ تُعْرَضُ صَلاتُنَا عَلَيْكَ وَقَدْ أَرَمْتَ؟ قَالَ: يَقُولُ: بَلِيتَ قَالَ:إِنَّ اللَّهَ تَبَارَكَ وَتَعَالَى حَرَّمَ عَلَى الأَرْضِ أَجْسَادَ الأَنْبِيَاءِ.(ابو داوُود)
📚Kutoka kwa Aws bin Aws (Radhwiyallaahu 'anhu)ambaye amesema:Mtume wa Allaah(swalallaahu 'alayhi wa sallaam) amesema:Hakika siku zenu zilizo bora mno ni siku ya Ijumaa, basi kithirisheni(zidisheni)kuniswalia siku hiyo, hakika Swalaah zenu huwa naletewa.(Maswahaba) wakasema: “Ee Mtume wa Allaah! Vipi Swalaah zetu unaletewa na ilihali wakati huo utakuwa umeshaoza?” Akasema:"Hakika Allaah Ameiharamisha ardhi kula viwiliwili vya Manabii".(Abu Dawud)
📚 Katika hadith hii imekuja kwa njia ya kutaja siku ya ijumaa haina maana kwamba siku zilizobakia kwamba mja asimswalie mtume kwani siki ya Ijumaa ni katika ubora pekee. Lakini kumswalia mtume ni Ibada ya siku zote. Na malipo yake ni makubwa kama; "Kupata uombezi wa mtume siku ya kiyama na kuwa karibu na yeye katika makazi ya peponi" kama ilivyothibiti katika hadith zinazozungumzia fadhila za kumswalia Mtume wetu kipenzi chetu swalallaahu 'alayhi wasallaam.
0️⃣4️⃣KUSOMA SURAH AL-KAHF
🤲0️⃣5️⃣KUOMBA DUA
📚 Amesema Allaah Subhaanahu wata'ala:
🤲وَقَالَ رَبُّكُمُ ٱدۡعُونِيٓ أَسۡتَجِبۡ لَكُمۡۚ,,,
🤲Na Mola wenu Mlezi anasema:"Niombeni nitakuitikieni"(ntakujibuni dua zenu),,,,,* Surah Ghafir, Ayah 60
📚Katika Ayaah hii Allaah ametuamrisha kumuomba na akatoa ahadi ya kujibu dua zetu. Lakini katika sunnah ya Allaah amejalia ubora katika kila kitu. Na katika nyakati na masiku pia amejalia zilizo bora zaidi kuliko nyingine. Miongoni mwa Siku bora katika kujibiwa dua, ni siku ya Ijumaa kama ilivyokuja katika hadith hapa chini.
📚 Amesema Mtume swalallaahu 'alayhi wasallaam:
📚عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ) أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) ذَكَرَ يَوْمَ الْجُمُعَةِ فَقَالَ:فِيهِ سَاعَةٌ لاَ يُوَافِقُهَا عَبْدٌ مُسْلِمٌ وَهُوَ قَائِمٌ يُصَلِّي يَسْأَلُ اللَّهَ تَعَالَى شَيْئًا إلاَّ أَعْطَاهُ إِيَّاهُ.....*(بخاري و مسلم)
📚Kutoka kwa Abu Hurayrah (Radhiyallaahu 'anhu) (amesema kwamba) Mtume wa Allaah (Swalallaahu 'alayhi wasallaam) ametaja Siku ya Ijumaa(kisha) akasema:"Humo mna saa(wakati) haimwafikii mja Muislamu akiwa amesimama anaswali anamwomba Allaah ta'aala kitu ila Anampa..."(Bukhaari na Muslim)
📚Saa ya kujibiwa dua iliyotajwa katika hadith hapo juu, kauli yenye nguvu imesemwa kuwa ni baada ya swalah ya 'Asr mpaka Swalah ya Magharib. Basi tenga mda wako japo kidogo umuombe Allaah katika fadhila zake. Wabillaahi tawfiiq

HATARI YA KUKOSA KUSWALI IJUMAA

📚 Amesema Allaah Subhaanahu wata'ala:
📚يَٰٓأَيُّهَا ٱلَّذِينَ ءَامَنُوٓاْ إِذَا نُودِيَ لِلصَّلَوٰةِ مِن يَوۡمِ ٱلۡجُمُعَةِ فَٱسۡعَوۡاْ إِلَىٰ ذِكۡرِ ٱللَّهِ وَذَرُواْ ٱلۡبَيۡعَۚ ذَٰلِكُمۡ خَيۡرٞ لَّكُمۡ إِن كُنتُمۡ تَعۡلَمُونَ
*📚Enyi mlio amini! Ikiadhiniwa Swalah siku ya Ijumaa, nendeni upesi kwenye dhikri ya Allaah(kuskiza khutbah), na wacheni biashara. Hayo ni bora kwenu, lau kama mnajua.*(Surah Al-Jumu'ah, Ayah:9)
📚Katika Ayaah hii, Allaah ameamrisha maamrisho ya swalah ya ijumaa kwa kuitaja siku ya ijumaa kwa jina. Na akahusisha na jambo lenye kuwashughulisha watu saana nalo ni biashara. Pamoja na kuwa kumetajwa biashara,lakini hapa kunaingia kila chenye kumshughulisha muisilamu na swalah na haijalishi kitu kwamba kitu hicho kinachomshughulisha muisilamu ni cha halali au ni cha haramu isipokuwa mambo ya dharura na yenye udhuru.

HATARI YA KUACHA SWALAH YA IJUMAA MAKUSUDI

📚Amesema Mtume swalallaahu 'alayhi wasallaam:
⚠️عن ابن عمر وأبي هريرة أَنَّهُمَا، سَمِعَا رَسُولَ اللَّهِ صلى الله عليه وسلم يَقُولُ عَلَى أَعْوَادِ مِنْبَرِهِ ‏ "‏ لَيَنْتَهِيَنَّ أَقْوَامٌ عَنْ وَدْعِهِمُ الْجُمُعَاتِ أَوْ لَيَخْتِمَنَّ اللَّهُ عَلَى قُلُوبِهِمْ ثُمَّ لَيَكُونُنَّ مِنَ الْغَافِلِينَ
⚠️Kutoka kwa Ibn 'Umar na Abii Hurayrah (Radhwiyallaahu ‘anhumaa) kwamba wamemsikia Mtume wa Allaah (Swalallaahu 'alayhi wa sallam)akiwa juu ya mimbari yake akisema: Wasiohudhuria Swalaah ya Ijumaa wabadilishe mwenendo wao huo au sivyo, Allaah Atawapiga mihuri katika nyoyo zao na watakuwa miongoni wa walioghafilika.(Muslim)
🌍Nini maana ya kupigwa mihuri?: Maana yake nikutiwa upofu wa moyo akawa mja hazinduki tena na mambo ya kheri na kuzidi kughafilika jambo ambalo linaweza kumpelekea kuwa na mwisho mbaya. Na tujitahidi japo kwa kujilazimisha. Nafsi inataka mazoezi na kupambana nayo kwani asili ya nafsi huwa haipendi kufanya mambo ya kheri bali ni yenye msukumo katika mambo maovu.
⚠️HALI IKISHA FIKIA HAPA, INAKUWA HATARI ZAIDI
📚Amesema Mtume swalallaahu 'alayhi wasallaam:
⚠️مَنْ تَرَكَ ثَلاَثَ جُمَعٍ تَهَاوُنًا بِهَا طَبَعَ اللَّهُ عَلَى قَلْبِهِ.(أحمد)
⚠️Atakayeacha Ijumaa tatu bila ya sababu yoyote, Allaah humpiga muhuri katika moyo wake.*(Ahmad)
📚Katika hadith hii,ni dalidli kwamba muisilamu anapopitwa na ijumaa tatu bila kuswali na wakati huo huo akiwa hana sababu ya kisheria,basi hali yake inakuwa mbaya. Kwani hadith hii imekuja kwa njia makhsusi ya ku idadisha jumla ya ijumaa ambazo hupelekea kupigwa muhuri kwenye moyo kwa yule mwenye kuziacha bila sababu.
⚠️Kumbuka kwamba huu ni ukumbusho.Na na ukiwa umekufikia,fikisha kwa wengine. Na jitahidi ukiwa ni miongoni mwa walioguswa na ukumbusho huu.Uyakumbuke maneno ya Allaah anapowazungumzia wale wenye kuupa mgongo ukumbusho wake Allaah.
📚Anasema Allaah Subhaanahu wata'ala:
⚠️وَمَنۡ أَعۡرَضَ عَن ذِكۡرِي فَإِنَّ لَهُۥ مَعِيشَةٗ ضَنكٗا وَنَحۡشُرُهُۥ يَوۡمَ ٱلۡقِيَٰمَةِ أَعۡمَىٰ
⚠️(Hapa Allaah anasema):"Na atakaye jiepusha na mawaidha(ukumbusho) yangu(mimi Allaah), basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu."(Surah Twaaha, Ayah:124)
📚Baada ya kufufuliwa kipofu atasemaje? Atasema hivi:
⚠️قَالَ رَبِّ لِمَ حَشَرۡتَنِيٓ أَعۡمَىٰ وَقَدۡ كُنتُ بَصِيرٗا
⚠️Aseme(mja aliyepuuza ukumbusho): Ewe Mola wangu Mlezi! Mbona umenifufua kipofu, nami(duniani) nilikuwa nikiona?.(Surah Twaaha, Ayah:125)
📚Kisha Allaah atamjibu:
⚠️قَالَ كَذَٰلِكَ أَتَتۡكَ ءَايَٰتُنَا فَنَسِيتَهَاۖ وَكَذَٰلِكَ ٱلۡيَوۡمَ تُنسَىٰ
⚠️(Allaah) atasema: Ndivyo hivyo. Zilikufikia ishara zetu(mawaidha), nawe ukazisahau(ukazipuuza); na hivyo leo unasahauliwa".*(Surah Twaaha, Ayah:126)
⚠️Hilo ndilo jibu la mwisho atakalopata mja mpuuzaji wa ukumbusho.

HUKUMU YA MAMBO MANANE YANAYOFUNGAMANA NA SIKU YA IJUMAA

1️⃣La kwanza: Kunyanyua mikono katikati ya khutbah wakati Imaam anaomba du'aa
Swali: Ni ipi hukumu ya kunyunyua mikono katika du´aa ya Khutbah ya Ijumaa?
Jibu: Haijuzu, kwa imamu na maamu, kunyanyua mikono katika du´aa ya siku ya Ijumaa. Isipokuwa katika du´aa ya kuomba kunyweshelezewa. Akimuomba mvua katika du´aa ya siku ya Ijumaa wanyanyue mikono yao. Mbali na du´aa ya kunyweshelezewa siku ya Ijumaa kusinyanyuliwe mikono.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
2️⃣La Pili: Kunyanyua Mikono kati kati ya khutbah mbili wakati khatwiyb ameketi chini kidogo.
Swali: Khatwiyb akiketi juu ya mimbari siku ya ijumaa na muadhini akaadhini unaanza wakati wa kuitikiwa du´aa. Je, ambaye ananyanyua mikono yake juu wakati adhaana inatolewa akatazwe?
Jibu: Ndio. Aelezwe kwamba hakuna dalili ya kunyanyua mikono juu wakati adhaana inatolewa. Ni jambo halina dalili. Mikono hainyanyuliwi katika ule wakati wa kuitikiwa du´aa siku ya ijumaa. Hakuna dalili juu ya hilo. Aombe pasi na kunyanyua mikono juu.
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/.../def.../files/igahssat.mp3
3️⃣La tatu: Kuchemua(kupiga chafya) na kujibu salaam kati kati ya khutbah
Swali: Mtu akitoa chafya wakati wa Khutbah ya ijumaa na akamhimidi Allaah, je aombewe kwa Allaah rehema?
Jibu: Hata salamu hatakiwi kujibiwa. Akija mtu na kutoa salamu asirudishiwe salamu, pamoja na kwamba kuitikia salamu ni wajibu. Wakati wa Khutbah ya ijumaa asirudishiwe. Tusemeje juu ya kumtakia rehema?
Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
0️⃣4️⃣.JAMBO LA NNE: NI UPI WAKATI BORA WA KUSOMA SURAH AL-KAHF SIKU YA IJUMAA? *(Mada-4)*
🎤 Aliulizwa Imaam Muhammad bin swalih bin'Uthaymin kuhusu wakati bora wa kusoma surah Al-Kahf siku ya ijumaa:⤵️⤵️⤵️
⬇️Swali: Inasihi kusoma Suurah “al-Kahf” usiku wa kuamkia ijumaa? Je, mtu huyu anapata fadhilah za kusoma Suurah “al-Kahf”?
➡️Jibu: Hapana. Kusoma Suurah “al-Kahf” kunakuwa siku ya ijumaa. Bora ni mtu asome baada ya jua kuchomoza. Una ruhusa ya kusoma kuanzia pale jua linapochomoza mpaka wakati wa kuzama kwa jua. Ukisoma wakati wowote, kuanzia pale wakati wa kuchomoza kwake mpaka wakati wa kuzama kwake, basi imesihi.
0️⃣5️⃣JAMBO LA TANO: WAKATI BORA WA KUOGA SIKU YA IJUMAA (Mada-5)
🎤Akaulizwa tena Imaam Muhammad bin swalih bin 'Uthaymin kuhusu wakati bora wa kuoga siku ya ijumaa:⤵️⤵️⤵️
⬇️Swali: Vipi mtu akioga josho la ijumaa usiku au baada ya alfajiri na akanuia kuwa ni josho la ijumaa?
➡️Jibu: Akioga kabla ya alfajiri hainufaishi kitu. Kwa sababu hapana shaka kwamba siku haijaingia. Akioga baada ya alfajiri inaweza kufaa. Lakini bora ni yeye kuoga baada ya jua kuchomoza.
📚Marejeo
👇👇👇
(Mada-5) Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (377)
(Mada-4) Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (69)
0️⃣6️⃣.Jambo la Sita: KUPONGEZANA SIKU YA IJUMAA KWA NENO"Jumaa Mubaraaka"
📚Swali: Vipi kuhusu kauli “Jum´ah mubaarakah”?
📚Jibu: Neno hili “Jum´ah mubaarakah” halina asli. Kupeana hongera kwa ajili ya Ijumaa ni jambo lisilokuwa na asli. Kupeana hongera inakuwa siku ya ´Iyd-ul-Fitwr na ´Iyd-ul-Adhwhaa. Ama kuhusu siku ya Ijumaa hapana.
Vilevile kuhusiana na mwanzoni wa kuingia mwaka mpya [wa Kiislamu] ni jambo halikuwekwa katika Shari´ah kupeana hongera kwa kuingia kwa mwaka wa Hijriyyah. Haya yote hayakuwekwa katika Shari´ah, bali ni katika Bid´ah.
0️⃣7️⃣Jambo la Saba:KUSOMA QUR-AAN KABLA YA IMAAMU KUINGIA
📚Swali: Je, ni halali msomaji akasimama siku ya ijumaa kabla ya imamu kuja na akija msomaji anakaa na baada ya hapo Khatwiyb anatoa Khutbah? Je, ni miongoni mwa adabu za ijumaa na Sunnah zake au ni katika Bid´ah munkari?
📚Jibu: Hatujui dalili yenye kufahamisha msomaji akasimama na kusoma Qur-aan siku ya ijumaa kabla ya imamu kuingia na watu wakamsikiliza na imamu akiingia msomaji anaacha kusoma. Asli katika ´ibaadah ni kwa mujibu wa Qur-aan na Sunnah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mwenye kufanya kitendo kisichokuwa ndani yake dini yetu, basi atarudishiwa mwenyewe.”
Ameipokea Muslim katika “as-Swahiyh” yake.
0️⃣8️⃣.Jambo la Nane:KUTOA DARSA KABLA YA KHUTBAH KWA WASIOJUA KIARABU
📚Swali: Katika msikiti wetu kwenye kituo cha Kiislamu huko (Marekani). Wasikilizaji ni ndugu zetu. Wana darsa kabla ya Khutbah ya siku ya ijumaa. Najua tangu hapo kitambo kwamba haifai kutoa darsa kabla ya Khutbah ya ijumaa.
🎤.Sheikh Albaaniy: Ndio.
📚Swali: Wanafanya hivo kwa sababu wasikilizaji hawazungumzi lugha ya kiarabu. Darsa inakuwa ni ile Khutbah imetafsiriwa kwa lugha ya kingereza. Je, jambo hilo linafaa?
🎤Sheikh al-Albaaniy: Unauliza juu ya hiyo Khutbah au darsa?
🎤Muulizaji: Kuhusu hiyo darsa(kwa lugha isiyo ya kiarabu) kabla ya Khutbah. Khutbah inatolewa kwa kiarabu.
🎤Sheikh al-Albaaniy: Darsa haijuzu. Hoja uliyotoa haitakasi kutoa darsa kabla ya Khutbah. Lakini hata hivyo wanaweza baada ya Khutbah na baada ya swalah au ndani ya Khutbah akawatangazia wasiokuwa waarabu wakamuuliza maswali au mambo yenye kutatiza baada ya swalah. Lakini kabla ya khutbah,darsa ni jambo lisilofaa.
🎤Muulizaji: Kama wanataka nitoe darsa kabla ya Khutbah ya ijumaa.
Al-Albaaniy: Haijuzu.
*📚Kumbuka,Uwajibu wa Ijumaa hauwahusu wanawake na wasafiri*
📚 Wabillaahi tawfiiq
📚MAREJEO
👇👇👇
(0️⃣8️⃣)Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
Marejeo: Silsilat-ul-Hudaa wan-Nuur (1023)
(0️⃣7️⃣)Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (2/357-358)
(0️⃣6️⃣)Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Imechapishwa: 01/05/2015
🌍Eneza kheri na kheri ienee kupitia mimi nawewe. Wabillaahi taw-fiiq
🌍Fikishia wengine usibadilishe chochote
📚Allaah subhaanahu wata'aala Anasema:
📚وَذَكِّرۡ فَإِنَّ ٱلذِّكۡرَىٰ تَنفَعُ ٱلۡمُؤۡمِنِينَ
📚Na kumbusha, Hakika ukumbusho huwafaa Waumini.(Surah Adh-Dhariyat, Ayah 55)

📚Na Mtume swalallaahu 'alayhi wasallaam Amesema:
📚بَلِّغُوا عَنِّي وَلَوْ آيَةً

📚Fikisheni kutoka kwangu japo Aayah moja.(Bukhaari)
🤲Tunamuomba Allaah atuwezeshe kufanya mema na kuacha maovu.
Wabillaahi tawfiiq





No comments:

Post a Comment

Type your comment here...

FEATURED

Can Muslims celebrate Christmas?

Can Muslims celebrate Christmas? There is no doubt that what is mentioned of celebrations is haram, because it is an imitation of the unbeli...